Twa kuwa wema kwa njia ya Kristo. Imeandikwa, 2Wakorintho 5:21 "Yeye asiye jua dhambi alimfanya kuwa adhambi kwa ajili yetu ili sisi tupeta kuwa haki ya Mungu katika yeye." Warumi 3:22 yasema "Ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa waote waaminio maana hakuna tofauti."
Wema wetu ukatika Kristo. Imeandikwa, Isaya 45:24 "Moja ataniambi, kwa Bwana peke yake iko haki na nguvu naam watu watamwendea yeye,..."
Hatuwi wema kwa kufanya mema. Imeandikwa, Isaya 64:6 Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu na matendo yetu yote ya haki yemekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa kama upepo uondoavyo"
Hatuna wema ndani yetu Mungu hutufanya kuwa wema. Imeandikwa, Zaburi 51:10 "Ee Mungu utuumbie moyo safi, uifanye safi roho iliyotulia ndani yangu."