Wasiwasi hausaidii. Imeandikwa katika Zaburi 37:8 "Ukomeshe hasira, uashe ghadhabu, usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya."
Hakuja haja ya kuwa na hofu.. Mungu yuko nasi. Imeandikwa katika Mathayo 6:31-33 "Msisumbukie, basi mkisema, tuleni nini? au tunyweni nini, au tuvae nini? kwa maana hayo yote mataifa huyatafuta kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Basi utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo yote mtazidishiwa."
Hatuwezi kuondoa hofu katika maisha yetu hadi tuwe na jambo jingine njema maombi. Imeandikwa Wafilipi 4:6- 7 " Msisumbukie kwa neno lo lote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu na amani ya Mungu ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu."
Kuwa na hofu ni kupoteza muda. Imeandikwa katika Luka 12:25-26 "Na yupi kwenu ambaye ajisumbua ambaye aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja basi ikiwa hamwezi hata neno lililo dogo kwa nini kujisumbua na hayo mengine?."
Mpe Mungu hofu zako. Imeandikwa katika 1Petro 5:7 "huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote kwa maana yeye hujishuguliza sana kwa mambo yenu."