Imani

Amini katika Bwana Yesu Kristo nawe utaokolewa. Imeandikwa katika Warumi 10:9 "Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka."

Mungu anasema tuko sawa tukimwamini Yesu. Imo katika Biblia; Mwanzo 15:6 "Ibrahimu akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hilo kuwa haki." Unalo fanya halipaswi kuwa tofauti na lile unaloliamini. Imeandikwa katika Torati 27:10 "Basi isikize sauti ya Bwana, Mungu wako, ufanye maagizo yake na amri zake nikuagizavyo leo."

Kuamini kwa kweli ni kuwa na uhusiano na Mungu. Imeandikwa katika Yohana 14:15. "Mkinipenda mtazishika amri zangu."

Niimani gani ambayo Mungu hukataa? Imeandikwa katika Yakobo 2:19 "Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka!"