Kahaba

Je kahaba ni nani? Imeandikwa, Mithali 9:13-18 "Mwanake pumbavu hupiga kelele ni mjinga hajui kitu hukaa mlangoni pa nyumba yake juu ya kiti mahali pa mjini palipoinuka. apate kuwaita wapitao njiani waendao moja kwa moja katika njia zao kila aliyemjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili, maji yaliyoibwa ni matamu na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza. Lakini huyo hajui yakuwa wafu wamo humo ya kuwa wageni wake wamo chini kuzimuni."

Mungu ameonya kufanya ukahaba. Imeandikwa, Mithali 5:3-14 "Maana mdomo wa Malaya hudondoza asali na kinywa chake ni laini kuliko mafuta lakini mwisho wake ni mchungu kuliko panga ni mkali kama upanga wa makali kuwili miguu yake inatelemkia mauti hatua zake zinashikamana nakuzimu hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima nji azake ni za kutanga-tanga wala hana habari basi wanangu nisikilizeni sasa wala msiache maneno ya kinywa changu itenge njia yako mbali naye wala usikaribie lango wa nyumba yake. usije ukawapa wengine heshima yako na wakorofi miaka yako wageni wasije wakashiba nguvu zakokazi zako zikawa ndani ya nyumba ya geni nawe ukaziobole siku zako za mwisho nyama yako na mwili wako utakapoangamia; ukasema jinsi nilivyo chukia maonyo na moyo wngu ukadharau kukemewa wala sikuisikia sauti ya walimu wangu wala sikuwategea sikio walionifundisha nalikua karibu na kuingia katika maovu yote katikati ya makutano na kusanyiko."

Munug anataka tuwe safi. Imeandikwa, 1 Wathesalonike 4:3 "Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kutakaswa kwenu muepukane na uasherati."

Mungu ametoa wokovu kwa makahaba. Imeandikwa, Mathayo 21:31-32 "Je! Katika hayo mawili ni nani aliye fanya mapenzi ya babaye wakamwabia yule wapili Yesu akawambia amini na nawaambia watoza ushuri na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. Kwa sababu yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki ninyi msimwamini la kini watoza ushuru na makahaba walimwamini nanyi hata mlipoona hamkutubu baadaye ili kumwamini."

Mungu alimwokoa Rahabu kahaba. Imeandikwa, Waebrania 11:31 "Kwa imani Rahabu, yule kahaba hakuanagaia pamoja na hao hakuangamia pamoja na hao walioasi kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelezi kwa amani."