Kisasi

Kulipisha kisasi ya paswa tumwashie Mungu. Imeandikwa Warumi 12:19 "Wapenzi sijilipizie kisasi bali ipiosheni ghadhabu ya Mungu maana imeandikwa kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa anena Bwana." Mithali 20:22 Yasema "Usiseme mimi nitalipa mabaya mgojee Bwana naye atakuokoa."
Tusilipishe kisasi kwa ajili ya upendo. Imeandikwa, Mathayo 5:38-39 "Mmesikia kwamba imenenwa jicho kwa jicho na jino kwa jino lakini mimi nawaambia msishindane na mtu mwovu lakini mtu akupigaye shavu la kuume mgeuzie la pili."

Usifurahi adui wako anapo kuwa na taabu. Imeandikwa Mithali 24:17-18 "Usifurahi adui wako aangukapo wala moyo wako usishangilie ajikwaapo Bwana asije akaliona hilo likamkasirisha akageuza mbali naye hasira yake."