Tunahitajika kufanya nini tunapo ona kosa kwa wengine imeandikwa Mathayo 7:1-2 "Msihukumu msije mkahukumiwa ninyi kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa."
Twatazamiwa kuwarejea watu makosa yao kwa moyo wa upole na kwa subira. Imeandikwa Waefeso 4:2 "Kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu mkichukuliana katika upendo."
Nivema kumweleza ndugu yako kosa? Imeandikwa Mathayo 18:15 " Na ndugu yako akikosea enenda ukamwonye wewe na yeye pekeyenu akikusukia umempata nduguyo."
Katika roho gani twapaswa kuwakosoa ndugu zetu? Imeandikwa Wagalatia 6:1-3 "Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mliowaRoho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe mchkuliane mizigo na kuitimiza hiyo sheria ya kristo maana mtu akijiona kuwa ni kitu naye si kitu ajidanganya nafsi yake."