Home / Masomo ya Biblia / Kueneza injili

Kueneza injili

Wakristo wanawezaje kujihusicha na uenezaji wa injili? Nilazima wenyewe wa ieneze injili hiyo Imeandikwa Mathayo "Ndipo alipowaambia wanafunzi wake mavuno ni mengi; lakini watendakazi ni wachache, basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake."

Kueneza injili ni kazi ya wakristo kote ulimwenguni. Imeandikwa Mathayo 28:19-20 "basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho mtakatifu na kuwafundisha kuyashika yote niliyo waamuru ninyi na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari."

Kueneza injili ya Yesu kuwe ni hali yetu ya maisha imeandikwa Wakolosai 1:26-29 "Siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake ambajinsio Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa nao ni kristo ndani yenu tumaini la utukufu amabaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu na kumfundisha kila mtu katika kila hekima yote tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika kristo Nami na jitaabisha kwa neno lilo hilo nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu."

Habari njema nilazima ihubiriwe kote kabla ya kurudi kwa Yesu. Imeandikwa Mathayo 24:14 "Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote hapo ndipo ule mwisho utakapokuja."

Siolazima uwena elimu ya juu kuweza kuhubiri injili imeandikwa 1Wakorintho 2:1-5 "Basi ndugu zangu mimi nilipokuja kwenu sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno wala kwa hekima maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu kristo naye amesulibiwa nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu bali kwa dalili za Roho na za nguvu iliimani yenu isiwekatika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu."

Tumeitwa tuwe mabalozi wa Yesu imeandikwa 2Wakorintho 5:20 "Basi tuwajumbe kwa ajili ya Kristo kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu."

Kueneza injili nikuzungumza kwaniaba yake Mungu na kuutangaza ukweli wake imeandikwa Marko 16:15 na Yohana 13:35 "Akawaambia enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri injili kwa kila kiumbe... hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mikiwa na upendo ninyi kwa ninyi."

Injili ni zaidi ya kuhubiri na ushuhuda imeandikwa Isaya 60:1 "Ondoka ukaangaze kwakuwa nuru yako imekujia na utukufu wa Bwana umekuzunguka. Imeandikwa Isaya 61:1 " Roho ya Bwana Mungu I juu yangu kwa sababu Bwana amenitia mafuta ni wahubiri wanyenyekevu habari njema amenituma ili kuwanganga waliovunjika moyo kuwatangazia mateka uhuru wao na hao walio fungwa habari ya kufunguliwa kwao."