Home / Masomo ya Biblia / Kumfunza mtoto

Kumfunza mtoto

Kuna umaana gani kumfunza mtoto mapema? Imeandikwa katika Mithali 22:6 "Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee."

Mungu anatarajia nini kutoka kwa wazazi wanapo wakuza watoto wao Imeandikwa Torati 6:6-7. "Na maneno haya ninayokuamuru leo yata kuwa katika moyo wako nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii nakuyanena uketipo katika nyumba yako na utembeapo njiani na ulalapo na uondokapo."

Mungu anawatazamia wazazi wawe wavumilivu. Imeandikwa katika Wakolosai 3:21 "Nanyi akina baba msiwachokoze watoto wenu wasije wakakata tamaa."

Mungu anatazamia mama awe vipi? Imeandikwa katika Mithali 31:26 "Hufumbua kinywa chake kwa heshima na sheria ya wema i katika ulimi wake."

Nidhamu ni namna yakuonyesha upendo kwa mtoto. Imeandikwa katika Mithali 13:24 "Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; bali ampendaye humrudi mapema."

Nidhamu njema humfunza mtoto Imeandikwa Mithali 29:15 "Fimbo na maonyo hutia hekima bali mwana aliyeachiliwa humuaibisha mamaye."

Sababu ya kumwathibu mtoto nikumfanya akuwe vema. Imeandikwa Waefeso 6:4 "Nanyi akina baba msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana."

Watoto hutoa matunda ya wazazi wao. Imeandikwa katika Kutoka 34:7 "Mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; Wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia hata kizazi cha tatu na cha nne."

Mungu ana tarajia matokeo gani kwa watoto? Imeandikwa katika Waefeso 6:1 "Enyi watoto watiini wazazi wenu katika Bwana maana hii ndiyo haki."