Home / Masomo ya Biblia / Kutongoza na kuonana kimwili

Kutongoza na kuonana kimwili

Yanayo tupasa kufanya wakati wa kutongozana. Imeandikwa, Warumi 13:13 "Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu si kwa ulafi na ulevi si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu."

Tunapo tongozana, tusije tuka onana kimwili. Imeandikwa, 1Wakorintho 6:13, 18, "Vyakula ni vya tumbo, na tumbo ni kwa vyakula lakini Mungu atavitowesha vyote viwili tumbo na vyakula lakini mwili si kwa zinaa...(18) bali kwa Bwana naye Bwana ni kwa mwili. Ikimbieni zinaa, kila dhambi aitendayo mwanadamu ni inje ya mwili wake ila yeye afanyaye zinaa hufanya juu ya mwili wake mwenyewe."

Jeweke safi. Imeandikwa, 1Yohana 3:3 "Na kila mwenye matumaini haya, katika yeye hujitakasa kaa yeye alivyo mtakatifu."

Tusije tukaumia sharti weka tamaa ya zinaa mbele za Bwana. Imeandikwa, 1 Wathesalonike 4:3-5 "Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kutakaswa kwenu muepukane na uasherati kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima. Sikatika hali ya tama mbaya kama mataifa wasio mjua Mungu."

Je kama umekwisha zini ufanye je? Kwanaza kubali kuwa umefanya dhambi. Imeandikwa, Zaburi 51:2-4 "Unioshe kabisa na uovu wangu unitakase dhambi zangu maana niejua mimi makosa yangu na dhambi yangu imbele zangu daima. Nime kutenda dhambi wewe peke yako na kufanya maovu mbele za macho yako wewe ujulikane kuwa una haki unenapo. na kuwa safi utoapo hukumu."

Pili omba msamaha wa dhambi zako. Imeandikwa, Zaburi 51:7-12 "Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko theluji unifanye kusikia furaha na shangwe mifupa ulioiponda ifurahi usitiri uso wako uzitazame dhambi zangu uzifute hatia zangu zote Ee Mungu uniumbie moyo safi uifanye upia roho iliyotulia ndani yangu, usinitenge na uso wako wala roho yako mtakatifu usiniondolee unirudishie furaha ya wokovu wako unitegemeze kwa roho ya wepesi."

Latatu, Amini kuwa Mungu amekusamehe dhambi zako. Imeandikwa, Zaburi 32:1-6 "Heri aliye samehewa dhambi na kusitiri makosa yake, Heri Bwana asiyemhesabia upotovu. Ambaye mwoyoni mwake hamna hila niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu mchana kutwa kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea jasho langu likakauka hata nikawakama nchi kavu wakati wa kaskazi Nalikujulisha dhambi zangu wala sikukufisha upotovu wangu nalisema nitayari maasi yangu kwa Bwana nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu kwa hiyo kila mtu mtauwa akuombe wakati unapopatikana hakika maji makuu ya furikapo hayata mfikie yeye."