Kutubu

Ni nani ambao wameitwa kutubu? Imeandikwa Luka 5:32 "Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu."

Tufanye nini baada ya kutubu? Imeandikwa, Luka 24:47 "Na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi kuanza tangu Yerusalemu."

Nitajuaje kuwa nimefanya dhambi? Imeandikwa, Warumi 3:20 "Kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria."

Je nifanye nini niweze kuokolewa? Imeandikwa, Matendo ya mitume 2:38, 16:31 "Petro akawaambia tubuni mkabatizwe kila moja kwajina la Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho takatifu. Wakamwambia, mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja na nyuba yako."

Kutubu ni zawadi kutoka kwa Mungu. Imeandikwa, Warumi 2:4 "Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake usijue yakuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu."
Na hisi vipi baada ya kutenda dhambi? Imeandikwa, Zaburi 38:18 "Kwa maana nitaugama uwovu wangu na kusikitika kwa dhambi zangu."

Kutubu kwa leta nini. Imeandikwa, 2 Wakorintho 7:10 "Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto bali huzuni ya dunia hufanya mauti."

Je Yesu husikiaje wakatu tunapo tubu? Imeandikwa, Luka 15:7 "Na waambia vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye kuliko ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu."