Home / Masomo ya Biblia / Kutumaini

Kutumaini

Umtumaini Mungu pekeyake. Imeandikwa, Mithali 3:5-6 "Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe katika njia zako zote mkiri yeye naye atayanyosha mapito yako."

Kumtumaini Mungu nikuamini kuwa atafanya yale ambayo ameahidi. Imeandikwa, Warumi 3:21-22 "Lakini sasa hakiya Mungu imedhihirika pasipo sheria imeshuhudiwa na torati na manabii ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Kristo Yesu kwa wote waaminio maana hakuna tofauti."

Amani ya kweli ipokwa kumwamini Mungu. Imeandikwa, Isaya 26:3 "Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu kwa kuwa amekutumaini."