Home / Masomo ya Biblia / Mafichoni

Mafichoni

Wakati mwingine twahitaji kwenda mafichoni wakatia wa uchungu. Imeandikwa, Mathayo 14:13 "Naye Yesu aliposikia hayo aliondoka huko katika chomboakaenda mahali pasipo watu, faraghani."
Mafichoni kwa weza kuwa pahali pema pakufanya maombi. Imeandikwa, Mathayo 14:23-24 "Naye alipokwisha kuaaga makutano alipanda mlimani faraghani kwanda kuomba na kulipokuwa jioni alikuwapo huko peke yake." Marko 1:35 yasema "Hataalfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu akaomba huko."

Kama Yesu alihitaji kwanda mafichoni je sisi twahitaji kiasi gani?. Imeandikwa, Luka 4:42 "Hata kulipokucha alitoka akaenda mahali pasipokuwa na watu makutano wakawa wakimtafuta-tafuta wakafika kwake wakataka kumzuia asiondoke kwao."