Malipo

Kufanya vitu upya. Imeandikwa, Kutoka 22:9 "Kila jambo la kukosana kama nila ng'ombe au la punda au la kondoo au la mavazi au la kitu cho chote kilichopotea, ambacho mtu mmoja asema ni chake, hilo jambo la watu wote wawili litaletwa mbele za Mungu naye atakayehukumiwana Mungu kuwani ni mkosa atamlipa mwenziwe dhamani yake mara mbili."

Twafanya dhambi mbele za Mungu tunapo danganya mtu wengine. Imeandikwa, Mambo ya walawi 6:2-5 "Mtu awaye ye yote akifanya dhambi na kuasi juu ya Bwana akamdanganya mtu mweziwe katika jambo la amana, au la mapatano au la kunyang'anya au kumwonea mwenziwe au kizubuz kitu kilichopotea na kutenda la uongo juu yake na kuapa kwa uongo katika mambo hayo yote moja wapo atakalolitenda mtu na kufanya dhambi kwalo ndipoitakapokuwa akiwa amefanya dhambi na kufanya hatia atarudisha hicho alicho kipata kwa kuonea au ile amana aliyowekewa au kitu kilichopotea alichokizubua yeye au kitu cho chote ambacho amekiapia uongo atakirudisha hata kwa utumilifu wake kasha ataongeza na sehemu ya tano zaidi juu yake naye atampa huyo mwenyewe siku hiyo atakayohukumiwa kuwa mwenye hatia. Kisha ataleta sadaka yake ay hatia..."

Mungu anataka tuombe msamaha na kulipa makosa yetu. Imeandikwa, Hesabu 5:5-7 "Kisha Bwana akanena na Musa na kumwambia uwaabie wana wa Israeli mtu mume au mke atakapofanya dhambi yo yote ifanywayo na binadamu, kumwasi Bwana, na mtu huyo akawa na hatia ndipowatakapo ungamana dhambi yao waliyoifanya naye atarudisha kwa hatia yake kwa utimilifu wake tena ataongeza juu yake sehemu ya tano na kumpa huyo aliyekosea."