Home / Masomo ya Biblia / Mapendeleo

Mapendeleo

Mungu hana mapendeleo imeandikwa Matendo ya mitume 10:34Petero akafumbua kinywa chake akasema, hakika natambua yakuwa mungu hana mapendeleo."

Warumi 2:11 yasema "Kwa maana hakuna mapendeleo kwa Mungu."

Kwa nini mungu anachukizwa na mapendeleo? Imeandikwa Malaki 2:9 "Kwasababu hiyo mimi naamini nimewafanya ninyi kuwa kitu chakudharauliwa na unyonge mbele ya watu wote kama ninyi msivyosishika njia zangu bali mmewapendelea watu katika sheria."

Mapendeleo ya toaumaana wa watu ambao yesu aliwafia pia inaonyesha kutomjua mungu. imeandikwa Yakobo 2:1-4 "Ndugu zangu imani ya Bwana yesu kristo Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendeleo watu maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhabu na mavazi mazuri kasha akaingia na maskini mwenye mavazi mabovu nanyi mkistahi yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia, keti wewe hapa mahali pazuri na kumwambia yule maskini simama wewe pale au keti munguuni pangu, Je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?."

Nijambo la hatari an lisilo la hekima kuonyesha mapendeleo haswa katika familia imeandikwa Mwanzo 37:3-4 "basi Isiraeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee wake akamfanya kanzu ndefu ndugu zake wakona yakuwa baba yao anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia wala hawakuweza kusema naye kwa imani."