Home / Masomo ya Biblia / Matendo Bila Imani

Matendo Bila Imani

Matendo bila imani ni hali ya kuweka sheria kuwa ya muhimu kuliko Mungu na mahiji ya watu. Imeandikwa, Mathayo 12:9-10 "akaondoka huka akaingia katika sinagogi lao na tazama yumo mtu mwenye mkono umepooza wakamuuliza wakisema ni halali kuponya watu siku ya Sabato? wapate kumshitaki akawaaambia ni mtu yupi miongoni mwenu kondoo mmoja na yule koondo ametumbukia shimoni siku ya Sabato asiyemshika akamwopoa?."

Matendo bila imani ni sawa na utumwa. imeandikwa, Wagalatia 4:8-9 "Lakini wakati ule kwa kuwa hamkumjua Mungu mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu bali sasa mkisha kumjua Mungu au zaidi kujulikana na Mungu kwa nini kuyarejea tena mafundisho mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge yenye upungufu ambayo mnataka kuyatumikia tena mnashika siku za miezi na nyakati na miaka."

Matendo bila imani huvutia lakini huharibu. Imeandikwa, Wakolosai 2:23 "Mambo hayo yana onekana kana kwamba yana hekima katika namna ya ibada mliyo jitungia wenyewe na katika kunyenyekea na katika kuutawala mwili kwa ukali lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili."

Tunaokolewa kwa imani bali si kwa matendo. Imeandikwa, Waefeso 2:8-10 "Kwa maana mmeokolewa kwa neema kwa njia ya imani abayo hiyo haikutokana na nafsi zenu ni kipawa cha Mungu wala si kwa matendo mtu awaye yote asije akajisifu, maana tu kazi yake tuliumbwa katika Kristo Yesu tutende matendo mema ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo."