Mateso

Maisha ya mkrito si maisha rahisi. Imeandikwa, Mathayo 5:11-12, "Heri ninyi watakapowashutukumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo kwa ajili yangu furahini na kushangilia kwa kuwa dhawabu yenu ni kubwa mbinguni kwa maana ndivyo walivyo waudhi manabii waliokuwa kabla yenu." na 2Timotheo 3:12-14 yasema "Naam na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika kristo Yesu wataudhiwa lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea na kuzidi kuwa waovu wakidanganya na kudanganyika bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa kwa maana unajua ni akina nani wali jifunza kwao."

Mateso hayaishi milele. Imeandikwa, 1Petro 5:10 "Na Mungu wa neema yote, aliye waitakingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo mkisha kuteswa kwa muda kidogo yeye mwenyewe atawatengeneza na kuwadhibitisha na kuwatia nguvu."

Kuna ahadi kwa wale wanao teswa na jamaa yao. Imeandikwa, Mathayo 19:29 "Na kila mtu aliye achawana nyumba au ndugu wakiume au wakike au baba au mama au mtoto au mashamba kwa ajili ya jina langu atapokea mara mia na kuuridhi uzima wa milele."

Mateso hutusaidia kukuwa kiroho. Imeandikwa, yakobo 1:2-3 "Ndugu zangu hesabunu yakuwa ni furaha tupu mkiangukia katika majaribu mbalimbali mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta sahuri."