Neema

Wakovu huja kwa neema na ni zawadi kutoka kwa Mungu. Imeandikwa Waefeso 2:8-9 "Kwa maana mmeokolewa kwa neema kwa njia ya imani amabayo hiyo haikutokana na nafsi zenu ni kipawa sha Mungu wala sikwa matendo, mtu awaye yeyote asije akajisifu."

Je neema hutupilia mbali sheria za Mungu? Imeandikwa Warumi 3:31, "Basi je! twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? hasha! kinyume cha hayo twaithibitisha sheria."

Neema ya Mungu ndio tumaini letu. Imeandikwa Nehemia 9:31 "Ila kwa neema zako nyingi hukuwakomesha kabisa, wala kuwasha kwa maana wewe u Mungu mwenye neema, mwenye rehema

Neema ya Mungu hufanya wokovu uwezekane. Imeandikwa Waefeso 1:7-8 "Katika yeye huyo kwa damu yake tunao ukombozi wetu masamaha ya dhambi sawasawa na wingi wa neema yake naye alituzidishia hiyo katiaka hekima yote na ujuzi."

Neema ya Mungu ina subira imeandikwa Warumi 2:4 "Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?."