Rehema

Bwana ni mwenye huruma. Imeandiikwa, Isaya 30:18 " Kwa ajili yahayo Bwana atangoja ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa ili awarehemu kwa maana Bwana ni Mungu wa hukumu, heri wote wamwongojao."

Zaburi 103 :13 yasema "Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao." Mika 7:18 yasema "Ninani aliye Mungu kama wewe mwenye kusamehe uovu na kuliachilia kosa la watu urithi wake wa watu walio salia? hashiki hasira yake milele kwa maana yeye hufurahia rehema."

Wakati tunapo mkosea Mungu tunashuhudia rehema za Mungu. Imeandikwa, Zaburi 6:2 "Bwana unufadhili maana ninanyauka Bwana uniponye mifupa yangu imefadhaika."

Wenye kujivuna hawashuhudii rehema za Mungu. Imeandikwa, Luka 18:13-14 "Lakini yule mtozaushuru alisimama mbali wala hakudhubutu kuinua macho yake mbinguni bali alijipiga-piga kifua akisema ee Munugu uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana ajikwezaye atadhiliwa naye ajidhiliye atakwezwa."