Tabaka

Wahurumie wale ambao hawawezi kukulipa. Imeandikwa, Luka 14:13-14 "Bali ufanyapo karamu uwaite maskini vilema, viwete, vipofu nawe utakuwa heri kwakuwa hao hawana cha kukulipa kwa maana utalipwa kwa ufufuo wa weneye haki."

Tusitengeneze tabaka katika mwili wa Kristo. Imeandikwa, Wagalatia 2:6 "Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo (walivyo kuwa vyo vyote ni mamoja kwangu Mungu hapokei uso wa mwanadamu ) nasema hao wenye sifa hawakuniongezea kitu."

Faida ipatikanayo kwa sababu ya matabaka haikubaliwi kwa wenye haki. Imeandikwa, Yakobo 2:8-9 "Lakini mkitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyo andikwa mpende jirani yako kama nafsi yako mwatenda vema bali mkiwapendelea watu mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji."

Katika macho ya Mungu sisi sote tu sawa sawa. Imeandikwa, Mathayo 20:25-28 "Lakini Yesu akawaita mwajua yakuwa wakuu wa mataifa huwatawala kwa nguvu na wakubwa huwatumikisha lakini haitakuwa hevyo kwenu bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu na awemtumishi wenu na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awemtumwa wenu. kama vile mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa bali kutumika na kutoa nafsi yake iwe fidia ya kweli."