Mungu anatufahamisha vipi kuhusu uhai (kiumbe kilicho tumboni mwa mama)?. Binadamu ana umuhimu kabla ya kuzaliwa. Imeandikwa katika Yeremia 1:5 "Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa nime kuweka kuwa nabii wa mataifa."
Mungu anatenda kazi na kiumbe ambacho hakijazaliwa kikiwa kingali tumboni. Imeandikwa katika Zaburi 139:13-14. "maana wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, uliniunga tumboni mwa mama yangu. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, na nafsi yangu yajua sana." Imeandikwa katika Kutoka 20:13, "usiue". Mungu ametuonya kutotoa uhai wa mtu mwingine.