Udhaifu

Ni kwa udhaifu wetu ndipo tunaweza kufahamu uweza wa Mungu. Imeandikwa, 2Wakorintho 12:9 "Naye akaniambia neema yangu ya kutosha maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi ili uweza wa Kristo ukae juu yangu."

Ni vema kuwapa moyo walio dhaifu. Imeandikwa, Warumi 14:1 "Yeye aliye dhaifu wa imani mkaribisheni walkini msimhukumu mawazo yake."

Mungu aweza kuwatumia hao wadhaifu ikiwa watakaa pamoja naye. Imeandikwa, 1Wakorintho 1:27 "Bali Mungu aliyachangua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu."