Kufuata mpango wa Mungu ndio hali bora ya kuzuia magonjwa. Imeandikwa, Kutoka 15:26 "Akawaambia, kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana Mungu wako na kufafanya yaliyoelekea mbele zake na kutega masikio uiskie maagizo yake na kuzishika amri zake mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyo yatia wamisiri; kwa kuwa mimi ndimi Bwana Mungu wako nikuponyaye."
Kumwabudu Mungu ni kuwana uhuru katika magonjwa. Imeandikwa, Kutoka 23:25 "Nanyi mtamtumikia Bwana Mungu wenu naye atakibariki chakula chako na maji yako; nami nitakuondole magonjwa kati yako."
Yesu alikuwa na uwezo wa kuponya. Imeandikwa, Mathayo 4:23-24 "Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote akiwafundisha katika masinagogi yao na kuihubiri habari njema ya ufalme na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu. Na habari zake zikaenea katika sehemu yote wakamletea walio kuwa hawajiwezi walio shikwana maradhi mbalimbali na mateso wenye pepo na wenye kifafa, na wenye kupooza akawaponya."
Uponyaji hutoka kwa Mungu. Imeandikwa, Yeremia 17:14 "Uniponye Ee Bwana nami nitaponyeka uniokoe nami nitaokoka kwa maana wewendiwe uliye sifa zangu."
Kuweza kupona nivema kufuata mpango wa Mungu. Imeandikwa, Yakobo 5:14-16 "Mtu wakwenu amekuwa hawezi? na awaite wazee wa kanisa nao wamwombee na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana na kulekuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule na Bwana atamwinua hata akiwa amefanya dhambi atasamehewa ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuobeana, mpate kuponywa kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii."
Hakutakuwa na magonjwa mbinguni. Imeandikwa, Isaya 33:24 "Wala hapana mwenyeji atakaye sema, mimi ngonjwa; watu wakaao humo watasaehewa uovu wao."