Home / Masomo ya Biblia / Ukamilifu

Ukamilifu

Ukamilifu ni tendo ambalo twastahili kufanya. Imeandikwa, Mathayo 5:48 "Basi ninyi mtakuwa wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu."

Ukamilifu ni hali ya kusikiliza, kukua na kuelimika tukiwezeshwa na Yesu. Imeandikwa, Wakolosai 1:28 "Amabaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu na kufundisha kila mtu katika hekima yote tupate kumletea kila mtu mtimilifu katika Kristo."

Ukamilifu utafika ukingo wakati Yesu atakaporudi. Imeandikwa Juda 1:24-25 "Yeye awzaye kuwalinda ninyi msijikwae na kuwasimamisha mbele ya utakatifu wake bila mawaa katika furaha kuu. Yeye aliye Mungu pekee mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu utukufu una yeye na ukuu na uwezo na nguvu tangu milele na sasa na hata milele amina."