Ukarimu

Ukarimu nimoja wapo ya utumishi kwa Mungu Imeandikwa. Mwanzo 18:3-5 "Akasema Bwana Mungu kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipatie sasa mimi mtumwa wako na yaletwe maji kidogo mkanawe minguu mkapumzike chini ya mti huu nami nitaleta chakula kidogo mkaburudishe moyo baadaye mwendelee, iwapo mmemjua mtumwa wenu wakasema haya, fanya kama ulivyosema."

Kukubali ukarimu hufanya wengine kufanya wema. Imeandikwa. Luka 10:7 "Basi kaeni katika nyumba iyo hiyo mkila na kunywa vya kwao maana mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake msihame hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii."

Ukarimu ni zawadi inayo kuwa kwa mazoea. Imeandikwa. Warumi 12:13 "Kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi."

Kufanya ukarimu twaweza kuwa tuna wakaribisha malaika. Imeandikwa. Waebrania 13:2 "Msisahao kuwafadhili wageni maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua."