UKIMWI

Tuwachukulieje watu wenye UKIMWI? Imeandikwa katika Wagalatia 4:14 "Na jaribu lililo wapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu."

Kama tuna nia ya kusamehewa lazima nasi tuwasamehe waliotukosea. Imeandikwa Mathayo 6:15, "Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu."

UKIMWI haupatikani tu kwa sababu ya anasa, bali kwa kutii amri za Mungu magonjwa yote ya zinaa yaweza kuzuilika. Imeandikwa katika Kutoka 20:14 "usizini." Walawi 18:22. "Usilale na mwanamume mfano wakulala na mwanamke; ni machukizo."