Utulivu

Mungu huogea katika utukalivu na ukimia Imeandikwa, 1Wafalme 19:11-13 "Akasema toka, usimame limani mbele za Bwana na tazamia BWANA akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima ukaivunja vinja miamba mbele za Bwana, lakini Bwana hakuwamo, katika upepo ule, na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini Bwanahakuwamo katika lile tetemeko la nchi, na baada ya tetemekola nchi kukawana moto, lakini Bwana hakuwamo katika moto ule, na baada ya moto sauti ndogo ya utulivu. Ikawa Eliya aliposikia alijufunika uso wake katika mavazi yake akatoka akasimama mlangoni wa upango. Na tazama sati ikamjia kusema, unafanya nini hapa, Eliya.?"

Twaweza kuona utukufu wa Mungu kwa utulivu. Imeandikwa, Zaburi 46:10 "Acheni, mjue ya kuwa mimi ni Mungu. Nitakuzwa katika mataifa nitakuzwa katika nchi."

Kuna nguvu katika utulivu. Imeandikwa, Isaya 30:15 "Kwa maana Bwana Mungu, mtakatifu wa Israeli asema hivi kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini lakini hamkukubali."

Utakatifu waleta utulivu na amani. Imeandikwa, Isaya 32:17-18 "Na kazi ya haki itakuwa amani na mazao ya haki utulivu na matuaini daima."

Utulivu na kuongesha unyenyekevu mbele za Mungu. Imeandikwa, Habakuki 2:20 "Lakini Bwana yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake."