Utunzi

Yesu alifunza hali bora ya utunzi Imeandikwa Luka 14:13-14 "Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema viwete, vipofu, nawe utakuwa heri kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa kwa ufufuo wa wenye haki."

Mungu anatazamia sisi tuwatunze wagonjwa na wenye taabu. Imeandikwa katika Wagalatia 4:14 "Na jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu."

Tunapowahudumia wenzetu tunamhudumia Mungu. Imo katika Mathayo 25:40 "Mfalme akajibu akawaambia, Amin nawaambia kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo mlinitendea mimi."