Uwepo

Twawezaje kujua Mungu yupo karibu au pamoja nasi? Imeandikwa, Zaburi 27:4 "Neno moja nimelitaka kwa Bwana nalo ndilo nitakalolitafuta nikae nyumbani mwa Baba sikuzangu zote za maisha yangu niutazame uzuri wa Bwana na kutafakari hekaluni mwake."

Kuwapo kwa Mungu hufahamika wakati wataabu. Imeandikwa, Zaburi 34:18-19 "Bwana yukaribu nao walio vunjika moyo na walio pondeka roho huwaokoa mateso ya mwenye haki ni mengi lakini Bwana humponya nayo yote."

Kuwapo kwa Mungu hujulikana wakati wa mateso. Imeandikwa, Zaburi 140:12-13 "Najua ya kuwa Bwana atamfanyia mnyonge hukumu na wahitaji haki yao hakika wenye haki watalishukuru jina lako wenye adili watakaa mahali ulipo wewe."