Wakili

Wakristo wastahili kuwa waakilishi wa Yesu Kristo. Imeandikwa, 2Wakorintho 5:20 "Basi tu wajube kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu."

Maisha ya mkristo ni kama barua iliyo wazi. Imeandikwa, 2Wakorintho 3:2-3 "Ninyi ndinyi barua yetu iliyoandikwa mioyoni mwetu inajulikana na kusomwa na watu wote mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu iliyoandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai si katika vibao vya mawe ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama."