Waume

Ni mafunzo gani tunayo yapata katika biblia kuhusu mabwana? Kazi kuu ya mabwana ni kuwapenda wake zao. Imeandikwa, Waefeso 5:25 "Enyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake."

Waume lazima tuwape heshima wake wao. Imeandikwa, 1Perto 3:7 "Kadhalika ninyi waume kaeni na wake zenu kwa akili na kumpa mke heshima kama chombo kisicho na nguvu na kama waridhi pamoja wa neema ya uzima kusudi kuomba kwenu kuzuiliwe."