Wokovu

Mungu ametupa wokovu kupitia kwake Yesu Kristo. Imeandikwa, Mathayo 1; 21 "Naye atazaa mwana naye atamwita jina lake Yesu maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao."

Wokovu wamaanisha kuwa na uzima wa milele tukiwa na uhusiano a Mungu. Imeandikwa, Yohana 17:3 "Na uzima wa milele ndiyo huu wakujue, wewe ndiye Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma." Yohana 3:16 yasema Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanwe pekee ilikila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele."

Kuna njia moja ya uzima wa milele nayo si rahisi. Imeandikwa, Mathayo 7:13-14 "Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba maana lango ni mpana na njia ni pana iendayo upotovuni nao niwengi waingiao kwa mlango huo bali wango ni mwembamba na njia imesonga iendayo uzimani nao waionayo ni wachache."

Wokovu ni zawadi. Imeandikwa, Waefeso 2:8-9 "Kwa maana mmeokolewa kwa neema kwa njia ya imani ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu ni kipawa cha Mungu wala si kwa matendo mtu awaye yote asije akajisifu."

Kupoke wokovu ni jambo lilo kuu na la kibinafsi na kutubu dhambi. Imeandikwa, Matendo ya mitume 2:37-38 "Walipo yasikia hayo waka chomwa mioyo yao waka mwambia petero na mitume wengine tutendeje ndungu zetu? Petro akawaambia tubuni kabatizwe kila moja kwa jina lake Yesu kristo mpate ondoleo la dhambi."

Kupokea wokovu ni rahisi na la kibinafsi. Imeandikwa Warumi 10:8-10 "Lakini yanenaje? lile neno likaribu nawe katika kinywa chako na katika moyo wako yaani nilile neno la imani tulihubirilo kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako yakuwa ni Bwana na kuliamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu utaokoka Kwa maana katiaka moyo mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa hukiri hata kupata wakovu."