Zawadi

Mungu humlipa mtu anaye fanya kazi kwa kujinyima bila kujionyesha. Imeandikwa, Mathayo 6:1 "Agalieni msifanye wema wenu machoni pa watu kusudi mtazamwe na wao kwa maana mkifanya kama hayo hampati dhawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni."

Mungu hutupa zawadi kwa wingi. Imeandikwa, Mathayo 19:29 "Na kila mtu aliye asha nyumba au ndugu wa kike au wa kiume au baba au mama au watoto au mashamba kwa ajili ya jina langu atapokea mara mia na kuuridhi uzima wa milele."

Mungu anatuletea zawadi. Imeadikwa, Ufunuo 22:12 "Tazama naja upesi na ujira wangu upamoja nami kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo."