Adui

Tunapaswa kuwa tendea vipi maadui wetu? imeandikwa Luka 6:27-36 "Lakini nawaambia ninyi mnaosikia wapendeni adui zenu watendeeni mema wele ambao wawachukia ninyi wabarikieni wale ambao wawalani ninyi waombeeni wale ambao waonea ninyi akupigae shavu moja mgeuzie lapili naye akunyang'anyaye joho lako usimzuilie na kanzu mpe kila akuombaye na akunyag'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie nakama mnavyo taka watu wawatendee ninyi watendeeni vivyo hivyo

Maana mkiwapenda wele wawapendao ninyi mwaonyesha fadhili gani? kwa kuwa hata wenye dhambi wawapenda wale wawapendao nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema mwaonyesha fadhili gani? hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo. Na mkiwakopesha watu vitu huku mkitumaini kupata kitu kwao mwaonyesha fadhili gani? hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi ili warudishiwe vile vile basi wapendeni adui zenu tendeni mema na kukopesha msitumaini kupata malipo na dhawabu yenu itakuwa nyingi nanyi mtakuwa wana wa aliye juu kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasio mshukuru na weovu basi iweni na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma."

Tuwatendee maadui zetu kwa roho njema. Imeadikwa Mathayo 5:25 "Patana na mshitaki wako upesi wakati uwapo pamoja naye njiani yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi na kadhi akakupeleka kwa askari ukatupwa gerzani."

Usifurahi katika majonzi ya adui zako. Imeandikwa Medhali 24:17-18 "Usifurahi adui yako aangukapo; wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; Bwana asije akaliona hilo likamkasirisha akgeuzia mbali naye hasira yake."

Imeandikwa Warumi 12:20 "Lakini adui yako akiwa na njaa mlishe akiwa na kiu mnyeweshe maana ufanyapo hivyo utampalia makaa ya moto kichwani pake."

Mungu ametuahidi kutuhifadhi kutokana na maanui wetu imeandikwa Zaburi 18:48 "Hutniponya na adui zangu naam waniinua juu yao walioniinukia na kuniponya na mtu wa jeuri."