Afya

Kwa nini ni shugulike juu ya afaya yangu?. Imeandikwa, 1Wakorintho 6:19-20. "Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho mtakatifu aliye ndani yenu, mliye pewa na Mungu wala ninyi si mali yenu wenyewe maan a mlinunuliwa kwa dhamani sasa basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu."

Mungu anatutazamia nini? Imendikwa, 3Yohana 1:2 "Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo."

Je! Mungu aliahidi wanawairaeli kuwaondolea magojwa kwa njia gani?. Imeandikwa Kutoka 15:26 "Akwawaabia utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake na kutega masikio usikie maagizo yake na kuzishika amri zake imi sitatia juu yako maradhi yo yote nilivyowatia wamisiri kwa kuwa mimi ndimi Bwana nikuponyaye."

Je! Mungu aliwaahidi nini hapo awali?. Imeandikwa Kutoka 23:25 "Nanyi mtamtumikia Bwana Mungu wenu naye atakibarikia chakula chako na maji yako nami nitakuondolea ugonjwa kati yako."

Nani aweza kuponya?. Imeandikwa Zaburi 103:2-3 "Ee nafsi yangu umhimidi Bwana wala usizisahau fadhili zake zote akusamehe maovu yako yote akuponya magojwa yako yote."

Kuwa naafya njema lazima tuwe na kiasi na mapumziko. Imeandikwa Kutoka 20:8-10 "Ikumbuke siku ya sabato uitakase siku sita fanya kazi yako utenda mambo yako yote lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana Mungu wako siku hiyo usifanye kazi yo yote."

Je hasira huiharibu afya yangu? Imeandikwa Mithali 17:22 "Moyo uliyochangamka ni dawa nzuri bali roho iliyopondeka huikausha mifupa."

Kuwa na wasiwasi nje lakini si ndani ya roho. Imeandikwa, wafilipi 4:6-7 "Msijisumbue kwa neno lo lote bali katika kila neno kwa kuomba na kusali pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu na amani ya Munug ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Yesu Kristo."

Twaweza je kuzuia magonywa ya zinaa? Imeandikwa 1Wakorintho 6:18 "Ikimbieni zinaa kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake ila kila atendaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe." Kutoka 20:14 yasema "Usizini".

Je mwanadamu alipewa chakula gani kabla ya dhambi? Imeandikwa Mwanzo 1:29 "Mungu akasea tazama nimewapa kila mche utoao mbegu ulio juu ya uso wa nchi yote pia na kila mti amao matunda yake yana mbegu vitakuwa ndivyo chakula chenu."

Baada ya garika Mungu aliwapa nini watu kama chakula chao? Imeandikwa Mwanzo 9:2-4 "Kila mnyaa kastika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu na kila ndege wa angani pamoja na vitu vyote vilivyo katika ardhi na samaki wote wa baharini vimetiwa mikononi mwenu kila kiendacho kicho hai kitakuwa chakula chenu kamanilivyo wapa mboga za majani kadhalika nawapeni hivyo vyote bali nyama pamoja na uhai yani damu yake msile."

Lazima tujue ni ni tanalo paswa kula. Imeandikwa Mambo ya walawi 11:47 "Ili kupambanua ati ya hao walio najisi na hao walio safi na kati ya kiumbe kilicho hai ambacho cha liwa na hicho kilicho hai ambacho hakiliwi." (Tazama Kumbu kumbu la torati 11 kwa maelezo zaidi.)

Vitu vilivyo safi na najisi haikuwa ya wayahu tu. Imeandikwa, Mwanzo 7:1, 2 Bwana akawambia Nuhu ingia wewe na jamaa yako yote katika safina kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki bele zangu katika kizazi hiki katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba mume na mke na katika wanyama wasiso safi wawili wawili."

Utenga wa vitu vilivyo safi na najifi vyaendelea hadi wakati wa mwisho. Imeandikwa Isaya 66:15, 17 "Maana Bwana atakuja na moto na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli ili atoye malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao kwa maonyo kwa miali ya moto watu walewajitakaso na kujisafisha katika bustani nyuma yake aliye katikati wakila nyama na nguruwe na machukizo na panya watakoma pamoja asema Bwana."

Je! Danieli alionyesha mfano gani juu ya chakula. Imeandikwa, Danieli 1:8 Lakini Danieli aliajimu moyoni mwake yakuwa hatajitia unajisi kwa kula chakula cha mfalme wala kwa divai aliyo kunywa pasi akamwomba yule mkuu wa matoashi ampe ruhusa asijitie najisi... mst. 12.. Tafadhali utujaribu sisi watumishi wako mda wa siku kumi na watupe mtama tule na maji tunywe."

Je kwa nini tuwe na kiasi katika malazi yetu 1Wakorintho 10:31 "Basi mlapo na mnywapo au mtendapo neno lo lote fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu."

Je maandiko yasama nini kuhusu mvinyo. Imeandikwa, Mithali 20:1 "Mvinyo hudhihaki kileo huleta ugomvi na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima."

Je! Mvinyo waleta taabu? Imeandikwa Mithali 23:29-35 "Ni nani apigaye, yowe? ni nani aliyae ole? nani mwenye ugomvi? ni nani mwenye mguno? ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu ni nani aliye na macho mekundu ni wale wakao kwenye mvinyo waendao kutafuta divai ilivyochanganyika usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu litiapo bilauri rangi yake ishukapo taratibu mwisho wake huwa kama nyoka huchoma kama fira macho yako yataona mengine na moyo wako utatoa yaliopotoka naam utakuwa kama alalaye katikati ya bahari au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti utasema wamenichapa wala sikuumia wamenipiga wala sina habari nitaamka lini nitazidi kuitafuta tena."

Je! matokeo ya kula na kunywa zaidi. Imeandikwa, Mithali 23:20-21. "Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo miongoni mwao walao nyama na pupa."