Je! Bibilia yamanisha nini inaposema agano jipya baina yetu na Mungu?. Agano jipya ndiyo jibu katika uasi wetu. Imeandikwa Yeremia 31:33 "Basi agano hili ndilonitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile asema Bwana nitatia sheria yangu ndani yao na katika ioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao nao watakua watu wangu."
Agano jipya laja kwa njia ya Yesu Kristo. Imeandikwa, Luka 22:20 "Kikombo nadho vivyo hivyo baada ya kula akisema; kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu."
Agano jipya yamaanisha twaweza kwende mbele za Mungu bila mpatanishi kupitia kwake Yesu Kristo. Imeandikwa, Waebrania 7:22 "Basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi."
Kuna ondoleo la dhambi katika agano jipya. Imeandikwa, Waebrania 9:14-15 "Basi si zaidi damu ya Yesu Kristo, ambaye kwa roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kua sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? na kwa sababu hi ni mjumbe wa agano jipya ili mauti ikisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya liyokuwa chini ya agano la kwanza hao waliyo itwa waipokee ahadi ya uridhi wa milele."
Katika agano la kale watu wasaki kufanya nini? Imeandikwa Kutoka 24:3 "Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya Bwana na hukumbu zake zote watu wote wakajibu kwa sauti moja wakasema maneno yote aliyoyanena Bwana Mungu tutayatenda."
Mungu ameagiza kufanya nini katika agano jipya?. Imeandikwa, Waebrania 8:10 "Maana hili ndilo agano nitakalo agana na nyumba ya Israeli baada ya siku zile asema Bwana nitawapa sheria zangu katika nia zao na katika mioyo yao nitaziandika nani nitakuwa Mungu kwao."