Asili

Ulimwenguni iwezekanapo kufikiri kinachotakiwa tu ni dhana za mtu binafsi na jinsi mtu ahisivyo kuhusu swala lolote, je Biblia inataja nini kuhusu kanuni mahsusi? Zimo katika Biblia, imeandikwa katika Zaburi 111:4, 7, 8 "Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu Bwana ni mwenye fadhili na neema matendo ya mikono yake ni ya kweli na hukumu, maagizo yake yote ni amini, yamethibitika milele na milele, Yamefanywa katika kweli na adili."

Mungu habadiliki. Imeandikwa katika Malaki 3:6 "Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu ndiyo maana ninyi hamkuangamizwa enyi wana wa Yakobo."

Je! Neno la Mungu ni kweli? Imeandikwa katika Yohana 17:17 "Uwatakase kwa ile kweli neno lako ndiyo kweli."

Je! Neno la Mungu litabadilika? Imeandikwa katika Biblia, Zaburi 93:5 "Shuhuda zako ni amini sana utakatifu ndiyo uifaayo nyumnba yako, Ee Bwana milele na milele." Mathayo 24:35 yasema "Mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe."

Neno la Mungu litahukumu ulimwengu wakati wa hukumu. Imeandikwa, Yakobo 2:10-12 "Maana mtu awaye ye yote atakayeishika sheria yote ila akajikwaa katika neno moja amekosa juu ya yote kwa maana yeye aliyesema usizini, pia alisema, usiue. basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru."

Mungu atatuhukumu kwa matendo yetu. Imeandikwa, Warumi 2:6, 11 "Atakaye mlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu."