Ushirikiano wetu na Mungu hubalisha jinsi tunavyo fikiri. Imeandikwa, Warumi 12:2 "Wala msiifuatishe namna ya dunia hii bali mgeuzwe kwa kufanywa upiya nia zenu mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kupendeza na ukamilifu."
Kama wakristo twapaswa kuwa na mawazo kama yake Yesu. Imeandikwa, 1Wakorintho 2:15-16 "Lakini mtu warohoni huyatambua yote wala yeye hutambua liwi na mtu maana ninani aliyeifahamu nia ya Bwana amwelimishe? lakini sisi tunayo nia ya Kristo."
Mafikara ya mkristo lazima iwena tabia ya Kristo. Imeandikwa, Wafilipi2:5 "Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo ndani ya Kristo Yesu."
Mafikara ya mkristo lazima yawe wema. Imeandikwa, Wafilipi 4:8 "hatimaye ndugu zangu mambo yo yote yalkiyo ya kweli yo yote yaliyo staha yo yote yaliyo ya haki yo yote yaliyo safi yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema, ukiwapo wema wo wote ikiwapo sifa nzuri yo yote yatafakarini hayo."