Furaha

Furaha huja panapo Mungu. Imeandikwa. Zaburi 16:8-9 "Nimemweka BWANA mbele yangu daima, kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa. kwahio mwoyo wangu unafurahi nao utukufu wangu unashangilia naam mwili wangu utakaa kwa kutumaini."

Furaha huja kwa kuzitunza sheria za Mungu. Imeandikwa. Yohana 15:10-11 "Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu Kama mimi nilivyo zishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake hayo nimewaambia ilifuraha yangu iwe ndani yenu na furaha yenu itimizwe.

Furaha ni zawadi kutoka kwa roho mtakatifu. Imeandikwa. Wagalatia 5:22-23 "Lakini tunda la roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utuwema, fadhili, uwaminifu, upole, kiasi, juu ya mambo kama hayo hakuna sheria."

Twaweza kuwa na furaha katika mambo yote. Imeandikwa. Wafilipi 4:4 "Furahini katika BWANA sikuzote tena nasema furahini."