Heshima

Ni Mungu pekeyake huwapa watu heshima au madaraka. Imeandikwa Zaburi 75:6, 7 "Maana siko mashariki wala magharibi wala nyikani itokako hekima, bali Mungu nduye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu."

Nivema kupeana heshima sisi kwa sisi. Imeandikwa Warumi 12:10 "Kwa pendo la undugu mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu."

Kuwaheshimu wazazi ni amri ya Mungu. Imeandikwa. Kutoka 20:12 "Waheshimu baba yako na mama yako siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana Mungu wako."