Hofu

Twawezaje kuhistahimili hofu? Kwa kuwa na imani na mungu imeandikwa Isaya 41:10 " Usiogope kwa maana mimi ni pamoja nawe nawe usifadhaike kwa maana mimi ni mungu wako nitakutia nguvu naam nita kusaidia naam nita kushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu."

Wakati wa hofu usimwashe mungu. Imeandikwa Yoshua 1:9 "Je? Si mimi niliyekuamuru? uwehodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako."

Tusimwogope mungu imeandikwa 1Yahana 4:18 "Katika pendo hamna hofu lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu kwa maana hofu in adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo."
Tusiogope maafa ya dunia imeandikwa Zaburi 46:1-3 "Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, masaada utakoonekana tele wakti wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. maji yake yajapovuma na ku kuumuka ijapopepesuka milima kwa kiburi chake."

Usiwaogope wanadamu imeandikwa Waebrania 13:6 "Hata twadhubutu kusema Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa mwanadamu atanitenda nini?."

Usiogope srikali wala mataifa imeandikwa Kumbukumbu la torati 7:21 "Usiogope na kicho kwa sababu yao kwa kuwa Bwana mungu wako yu katikati yako Mungu mkuu mwenye utisho."
Usiogopo habari mbaya imeandikwa Zaburi 112:7-8 "Hataogopa habari mbaya; moyo wake u imara ukimtumaini Bwana Moyo wake umedhibitika hataogopa, hata awaone watesi wake wameshindwa."