Huzuni

Mungu ameahidi kutuondolea huzuni, kilio, kifo na shida zote. Imeandikwa, Ufunuo 21:4 "Nayeatafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena wala maombolezi wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita."

Mbiguni kutakuwa mahala pa furaha na amani milele. Imeandikwa, Isaya 35:10 "Nahao waliokombolewa na Bwana watarudi watafika sayuni, wakiimba na furaha milele itakuwa juu ya vichwa vyao na watapata kicheko na furaha kuzimu na kuugua zitakimbia."

Huzuni haidumu milele. Imeandikwa, Zaburi 30:5 "Maana ghadhbu zake ni zakitambo kidogo katika radhi yake mna uhai huenda kilio huja kukaa usiku lakini asubuhi huwa furaha."

Mungu atatuponya na huzuni zetu. Imeandikwa, Zaburi 147:3 "Huwaponya walio pondeka moyo na kuziganga jeraha zao."

Yesu ameahidi kutufariji. Imeandikwa, Yohana 14:16 "Nami nitamwomba Baba naye atawapa msaidizi mwingine ili akaye nanyi hata milele."

Kubali ahadi ya amani. Imeandikwa, Yohana 14:27," Amini nawaachieni amani yangu nawapa niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo msifadhaike mioyoni mwenu wala siwe na woga."
Tukiwa na matumaini ya ufufuo wa pili ya tupa amani. Imeandikwa, 1Wathesalonike 4:13-18 "Lakini ndungu hatutaki msi jue habari za waliolala mauti msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini, maana ikiwa twaamini yakwamba Yesu alikufa akafufuka vivohivyo nao walio lala katika Yesu Mungu atawaleta pamoja naye kwa kuwa twaambieni haya kwa neno la Bwana kwamba sisi tulio hai tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana hakika hatutawatangulia hao walio kwisha kulala mauti kwa sababu Bwana wenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na waliko na sauti ya malaika mkuu na parapanda ya Mungu Nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza, kasha sisi tulio hai tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili tumlaki Bwana hewani na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno haya."

Wafu wataishi tena. Imeandikwa, Yohana 5:28-29, "Msistaajabie maneno hayo kwa maana saa yaja ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake nao watatoka wale walio fanya mema kwa ufufuo wa uzima na wale walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu."