Ibada

Ni sala gani tunapaswa kumpa Mungu? Tunapaswa kumuendea kama rafiki imeandikwa Kutoka "Musa akamwambia Bwana angalia wewe waniambia wachukuwe watu hawa; nawe hukunijulisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. walakini umesema nakujua jina lako, nawe umepata neema mbele zangu basi sasa nakuomba ikiwa nimepata neema mbele zako unionyeshe njia zako nipate kukujua, ili nipate neema mbele zako ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako."

Nilazima tutoe moyo wetu wote tunapo fanya sala kwa mungu Imeandikwa 1Mambo ya nyakati 28:9 "Nawe suleimani mwangu mjue mungu wababa yako ukamtumikie kwa moyo mkamilifu na kwania ya kumkubali kwa kuwa Bwana hutafuta -tafuta mioyo yote na kuyatambua mawazo yote ya fikira ukimtafuta ataonekana nawe ukimwacha atakutupa milele."

Mathayo 12:30 unasema "Mtu aseye pamoja nami yu kinyume changu na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya."

Wanao mtafuta Mungu kwa mioyo yao yote huitwa "wenye kubarikiwa" imeandikwa Zaburi 119:2 "Hiri wazitiio shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wote."