Imani

Imani nini? Imeandikwa waebrania 11:1 "Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bana ya mambo yasiyoonekana."

Yesu ndiye mwanzo wa imani imeandikwa Luka 17:5 "Mitume wakamwambia Bwana tuongezee imani." Warumi 10:17 yasema "Basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo."

Imani ya haki ni kuamini yote ambayo Yesu ametutendea. imeandikwa Warumi 5:1 "Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na imani kwa Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu kristo."

Imani ni kuwana imani kwa Mungu katika mambo yote. imeandikwa Waebrania 10:38 "Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani naye akisita-sita Roho yangu haina furaha naye."

Imani dhaifu yaweza kuwa yenye nguvu Mungu akimsaidia imeandikwa Marko 9:24 "Mara babaye yule kijana akapaza sauti akasema Naamini nisaidie kutokuamini kwangu."