Maandiko ya tuambia ya kuwa Yesu alifufuka kutoka kwa wafu. Imeandikwa, Mathayo 28:5-6 "Malaika akajibu akawaambia wale wanawake msiogo ninyi; kwa maana najua ya mnamtafuta Yesu aliyemsulubiwa. Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema njoni mpatazame mahali alipolazwa."
Yesu alifufuliwa kama ilivyotabiriwa. Imeandikwa, 1Wakorintho 15:3-4 "Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kama yanavyo andikwa maaandiko na yakuwa alizikwa na ya kuwa alifufuka siku ya tatu kama yanenavyo maandiko."
Ufufuo wa Kristo ni kina cha ukweli wa imani ya wakristo. Imeandikwa, 1 Wakorintho 15:14-17 "Tena kama vile Yesu hakufufuka kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure naam na sisi tumeonekana kwa mashahidi ya uongo wa Mungu kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua ikiwa wafu hawafufuliwi maana kama wafu hawafufuliwi Kristo naye hakufufuka na kama Kristo hakufufuka imani yenu ni bure; mgalimo katika dhambi zenu."
Biblia yasemaje kuhusu ufufuo wetu. Imeandikwa, 1Wakorintho 15:12-14 "Basi ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona kati yenu husema ya kuwa hakuna kiyama katika wafu? lakini kama kuna kiyama ya wafu Kristo naye hakufufuka, bali kuhubiri kwenu ni bure na imani yenu ni bure."
Miili yetu itabadilishwa na haitaona mauti tena. Imeandikwa, 1Wakorintho 15:51-53 "Angalieni na waambia ninyi siri hatutalala sisi sote lakini tutabadilika, kwa dakika moja kufumba na kufumbua wakati wa parapanda ya mwisho maana parapanda italia na wafu watafufuliwa wasiwe na uharibifu nasi tutabadilika maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika nao hu wa kufa uvae kutokufa."
Kristo kufa kwake anauwezo wa kufufua na anauhusiano na wao walio wafu katika kiroho. Imeandikwa, Wafilipi 3:10 "Ili nimjue yeye na uwezo wakufufuka kwake na ushirika wa mateso yake nikifananishwa na kufa kwake." Wefeso 2:1, 4, 5 yasema "Ninyi mlikuwa wafu kwa makosa yenu na dhambi zenu, Lakini Mungu kwa kuwa ni mwingi wa rehema kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda hat wakati ule tulio kuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu alituhuisha pamoja na Kristo yani tumeokolewa kwa neema."