Home / Masomo ya Biblia / Kufundisha

Kufundisha

Funza watoto wako kuhusu Mungu kutokana na mafunzo ambayo umeyapata katika hali ya maisha yako. Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 6:7 "Nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani na ulalapo na uondokapo."

Funza kweli katika kizaki hiki kwani ndicho kimekaribia kwesha. Imeandikwa, Waamuzi 2:10 "Tena watu wote wakizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao kikainuka kizazi kingine nyuma yao ambacho hakikumjua Bwana wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli."

Kufunza ni kwema ikiwa kutakuwa na matunda mema. Imeandikwa, Mathayo 7:24 "Basi kila asikiaye maneno yangu na kuyafanya atafanikishwa na mtu mwenye akili aliye jenga nyumba yake juu ya mwamba."