Home / Masomo ya Biblia / Kufunga, kutokula

Kufunga, kutokula

Kufunga nini na inamaana gani katika maisha ya kiroho? imeandikwa 2Mambo ya nyakati 20:3 "Yehoshefati akaogopa, akauwelekeza uso wake amtafute Bwana akatangaza mbiu ya watu kufunga katika yuda yote."

Kufunga kunaonyesha hitaji letu kuu kwa Mungu imeandikwa Ezra 8:21 "Ndipo nikaamuru kufunga hapo penye mto Ahava ilitupatekujinyenyekeza mbele za Mungu na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili ya sisi wenyewe na kwaajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote."

Kufunga kusifanywe ili kujionyesha imeandikwa Mathayo 6:17-18 "Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani unawe uso; ili usionekane na mtu kuwa unafunga, ila na BABA yako aliye sirini na BABA yako aonaye sirini atakujazi."

Waweza kula chakula kido wakati unafunaga. imeandikwa Danieli 10:2, 3 "Katika siku zile mimi danieli nilikuwa nikiomboleza munda wa majuma matatu kamili sikula chakula kitamu wa nyama wala divai haikuingia kunywani mwangu wala sikujipaka mafuta kabisa hata majuma matatu yalipotimia."