Kujiua

Ingawaje maisha yako yaweza kuwa mabaya na yenye shida bila matumaini ya wakati ujao Mungu yu pamoj anawe Imeandikwa, 2Wakorintho 4:8-9 "Pande zote twadhikika bali hatusongwi, twaona shaka bali hatukati tamaa, twaudhiwa bali hatuashwi twatupwa chini bali hatuangamizwi.".

Unadhamani kuu kwa Mungu. Imeandikwa, Luka 12:6-7 "Je! Mashomoro watanao hawauwezi kwa senti mbili? wal hasauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote msiogope basi, bora niyni kuliko mashomoro wengi."

Mungu hufikiri juu yako na anakushugulikia. imeandikwa, Zaburi 139:17-18 "Mungu, fikira zako zina dhamani nyingi kwangu jinsi ilivyo kubwa jumla yake, kama ningezihesabu ninyingi kuliko mshanga niakapo ni kali paoja nawe."

Umeahidiwa maisha ya ajabu. Imeandikwa, Yeremaya 29:11 "Maana nayaju mawazo ninayowawazia ninyi asema Bwana ni mawazo ya amani na si ya mabaya kuwapa tumaini siku zenu za mwisho."

Mungu atakusaidia wakati mzigo wako ni mzito. Imeandikwa, Zaburi 55:22 "Umtwike mzigo wako naye atakutegemeza hatamwasha mwenye haki aondoshwe milele." Mathayo 11:28-30 yasema "Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha jitieni nira yangu mjifunze kwangu kwakuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo nanyi mtapata raha nafsini mwenu kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi."

Haipo pekeyako ukiwa unafikiri kujiua! Watu wengi katika bibilia walifikiri kujiua.. Imeandikwa, Hesabu 11:14-15 "Mimi siwezi kuwachukuwa watu hawa wote peke yangu, kwa kuwa ni mzigo zito sana wa kunishinda na kama ukinitenda hivi, na kuomba uniulie mbali kwa maba nimepata fadhili mbele ya macho yako nami ni yaone haya mashaka yangu." pia Elija alikumbwa na mzigo huu 1Wafalme 19:3-4 "Naye alipoona hayo aliondoka akaenda aihifadhi roho, yake, akafika Beersheba, mji wa Yuda akamwacha mtumishi wake huko. lakini yeye mwenyewe akaenda katika jangwa mwendo wa siku moja akaenda akaketi chini ya mretemu akajiombea roho yake afe, akasema yatosha, sasa Ee Bwana uniondoe roho yangu kwa kuwa mimmi si mwema kuliko baba zangu."

Ikiwa umekumbwa na hofu Mungu atakusaidia. Imeandikwa, Isaya 41:10 "Usiogope kwa maana mimi nipo pamoja nawe usifadhaike kwa maana mimi ni Mungu wako nitakutia nguvu naam nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu."

Mungu hatakuasha hata wengine wako wakikuasha. Imeandikwa, Zaburi 9:10 "Nao wakujuao jina lako wakutumaini wewe maana wewe Bwana, hakuwaacha wakutafutao." Zaburi 46:1-3 yasema "Munug kwetu ni kimbilio na nguvu msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari maji yake yajapovuma na kuumika ijapopepesuka milima kwa kiburi chake."

Mungu anataka kutupatia amani ya roho na mafikara. Imeandikwa, Yohana 14:27 "Amani na waachieni, amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama vile ulimwengu utoavyo msifadhaike mioyoni mwenu wala msiwena na woga." Yahona 16:33 yasema "Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu ulimwenguni mnayo dhiki, lakini jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu."

Kwa uwezo wa Mungu, jaribu kufikiri juu ya mabo yenge umuhimu na mambo mema. Imeandikwa, Wafilipi 4:8 "Hatimaye ndugu zangu mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki yo yote yaliyo safi yo yote yenye kupendeza yo yote yenye sifa njema ukiwapo wema wo wote ikiwapo sifa nzuri yo yote ya tafakarini hayo."

Ukiwa unasikiwa ukiwa peke yako na ukiwa kumbuka ya kuwa wewe unadhamani kuu kwa Mungu unamarafiki wano weza kukusaidia na kusikia shida zako.