Home / Masomo ya Biblia / Kukataliwa

Kukataliwa

Watoto wa Mungu watakataliwa na jamii yao na, marafiki zao. Imeandikwa, Marko 6:4 "Yesu akawaambia nabii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake mwenyewe na kwa jamaa yake na nyumbani mwake." Zaburi 27:10 yasema "Baba yangu na mama yangu wameniacha bali Bwana atanikaribisha kwake."

Yesu alionyecha uchungu wakati alipokataliwa na marafiki zake. Imeandikwa, Luka 13:34 "Ee Yerusalemu, Yerusalemu uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake wala hamkutaka."

Yesu alikataliwa, anajua uchungu wake. Imeandikwa, Isaya 53:3 "Alidharauliwa na kukataliwa na watu mtu wahuzuni nyingi ajua masikitiko nakama mtu amabaye watu humficha nyuso zao alidharauliwa wala hatukuhesabu kuwa kitu."

Twamkataaa Mungu tunapo kataa wokovu wake. Imeandikwa, Mathayo 21:42 "Yesu akawaambia hamkupata kusoma katika maandiko, jiwe walilolikataa waashi hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni neno hili limetoka kwa Bwana nalo ni ajabu machoni petu."

Naye mkataa Mungu hana hekima. Imeandikwa, Zaburi 14:1 "Mpubavu asema moyni mwake hakuna Mungu wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo hakuna atendaye mema."