Kulala

Tukijua Mungu yupo pamoja nasi twaweza kupumzika hata wakati wa dhiki. Imeandikwa, Zaburi 3:5 "Nalijilaza nikalala usingizi nikaamka kwa kuwa Bwana ananitegemeza."

Wakati hatuna usingizi twaweza kufiria jinsi Mungu alivyo nasi. Imeandikwa, Zaburi 63:6 "Ninapokukumbuka kitandani mwangu na kutafakari wewe makesha yote ya usiku."

Tutakuwa na ulinzi tukijua ya kuwa Mungu halali. Imeandikwa, Zaburi 121:2-4 "Msaada wangu ukatika Bwana aliyezifanya mbingu na nchi usiuache mguu wako usongezwe asisinzie akulindaye naam hata sinzia wala hatalala usingizi yeye aliye mlinzi wa Israeli."