Home / Masomo ya Biblia / Kumcha mungu

Kumcha mungu

Sheri ya kwanza ni kumuogopa Mungu imeandikwa Kumbukumbu la torati 10:12-13 "Na sasa Israeli Bwana mungu wako anataka nini kwako? umche Bwana mungu wako na kwenda katika njia zake zote na kumpenda na kumtumikia Bwana mungu wako kwa roho yako yote; kuzi shika amri za Bwana na sheria zake ninazokuamuru leoupate uheri."

Mungu huwafunza wale wanao mcha Mungu imeandikwa Zaburi 25:12 "Ni nani amchaye Bwana? atamfundisha katika njia anayoichagua."

Kumcha mungu kuna leta hekima imeandikwa Medhali 9:10 "Kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima, na kumjua mtakatifu ni ufahamu."

Kumcha mungu ni heri kuliko utajiri. Imeandikwa Medhali 15:16 "Kuwa na mali chache pamoja na kumcha Bwana; ni bora kuliko mali nyingi pamoja na taabu."

Kumcha Bwana ni kimbilio kwa watoto. Imeandikwa Medhali 14:26-27 "Kumcha Bwana ni tumaini imara; watoto wake watakuwa na kimbilio. Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima ili kuepukana na tanzi za mauti."